The House of Favourite Newspapers

Kill Marathon yazinduliwa jijini Dar

0

1Naibu Mkurugenzi wa Vijana, Habari, Utamaduni na Michezo, Alex Nkenyenge akisistiza jambo kwenye hafla hiyo.2Naibu Mkurugenzi wa Vijana, Habari, Utamaduni na Michezo, Alex Nkenyenge akisistiza jambo kwenye hafla hiyo.

3Mapaparazi kazini

4Meneja Masoko wa GAPCO, Caroline Kakwezi akieleza jinsi kampuni yake ambayo ni wadhamini wamashindano hayo itakavyotoa ofa ya usafiri na misosi kwa washiriki.

5Mashindano yakizinduliwa rasmi.

6Mkutano ukiendelea.

7Meneja wa Kinywaji kisicho na kilevi cha Grand Malt ambacho kitakuwa kikitumiwa na wakimbiaji wakiwa njiani sambamba na maji, Oscar Shellukindo akieleza jinsi kinywaji chake kilivyodhamini mashindano hayo.

Mashindano ya mbio za Kill Marathon ambayo yanatarajiwa kuanza kutimua vumbi Moshi mkoani Kilimanjaro, Februari 28 mwakani yamezinduliwa leo kwenye hafla iliyofanyika Hoteli ya New Afrika Jijini Dar es Salaam.
Akizungumza katika hafla hiyo, Naibu Mkurugenzi wa Wiraza ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Alex Nkenyenge amewapongeza wadhamini wakuu wa mashandano hayo kwa mara ya 14 mfululizo Kampuni ya Bia ya TBL kupitia bia yake ya Kilimanjaro.
Mkurungenzi huyo aliwapongeza wadhamini wengine wa mashindano hayo Kampuni ya mafuta ya GAPCO, Kampuni ya simu za mkononi ya Tigo, Shirika la ndege la Rwanda ‘RwandAir’ na wengineo kwa mchango wao wa kuendeleza mchezo huo hapa nchini.
Naye Mkurugenzi wa mbio hizo, John Bayo alisema washuindi wa mbio hizo watapimwa afya zao kuhakiki kama hakuna aliyetumia madawa ya kuongeza nguvu au kusisimua misuli.
Bayo amesema endapo mshindi atabainika kutumia madawa hayo atanyang’anywa ushindi.
Meneja wa Bia ya Kilimanjaro waandaji wakuu wa mashindano hayo, Pamela Kikuli amesema wanajivunia kampuni yake kuendelea kuyadhamini mashindano hayo kwa miaka 14 sasa na kuyapa umaarufu mkubwa.

PICHA : RICHARD BUKOS / GPL

Leave A Reply