The House of Favourite Newspapers

Kim Jong-un: Nipo Tayari Kukutana na Trump

KIONGOZI wa Korea Kaskazini, Kim Jong-un amesema nia yake ya kukutana na Rais wa Marekani Donald Trump ili kuzungumza na kufikia makubaliano iko palepale licha ya kauli yake aliyoitoa hivi karibuni iliyodhoofisha mpango huo.
Kim Jong-un amesema hayo baada ya mkutano wake wa kushtukiza wa juzi Jumamosi na Rais wa Korea Kusini, Moon Jae-in.
Trump alisitisha mkutano uliopangwa kufanyika Juni, 12 mwaka huu kuzungumzia mpango wa nuklia wa Korea Kaskazini, lakini juzi Jumamosi alibadili maamuzi yake na kusema kuwa mambo yanaendelea vizuri kuelekea mkutano huo.
Imeelezwa kwamba, Balozi wa zamani wa Marekani nchini Korea Kusini, Sung Kim, atafanya mazungumzo na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Korea Kaskazini kuhusu maandalizi ya mkutano, vyombo vya habari vya Marekani na Korea Kusini vimeeleza.
Mkutano huo ni matunda ya jitihada za kidiplomasia ambazo zilianza mwaka huu kujaribu kuondoa hali ya msuguano uliohofiwa kugeuka kuwa makabiliano ya kijeshi kati ya Korea Kaskazini, Korea Kusini na Marekani.
Credit:BBC.

Comments are closed.