The House of Favourite Newspapers

Kim Kardashian Avaa ‘Kimtindo’ Akitalikiana na Kanye West

0
Kim akiwa katika vazi maalum la kuvutia baada ya kuachana na mumewe.

KIM KARDASHIAN (40) jana (Alhamisi) alitoa picha zake kwenye mtandao wa Instagram akiwa katika nguo yenye rangi ya fedha inayoonyesha umbo lake la kuvutia.

 

Picha hizo alizitoa katika kupromoti marashi (pafyum) aina ya KKW ya kampuni ya Metallic Hearts aliyokuwa akihusika nayo.

Nyota huyo aliandika katika mtandao: “Pafyum tatu za kuvutia zikiwa katika kichupa chenye taswira ya moyo, pamoja na zile za  KKW Hearts, yaani  BAE, BFF & WIFEY ni kwa  ajili ya Siku ya Wapendanao (Valentine’s Day) vikiwa ni zawadi kwako na au uwapendao! ”

Picha hiyo inakuja baada ya kiitwacho kutalikiana na Kanye, 43.

Imeripotiwa kwamba wawili hao wameacha kabisa kwenda kupata ushauri kuhusu ndoa yao na kwamba Kanye anataka talaka ifanyike wiki hii.

Mwanzoni mwa mwzi huu, vyanzo vilisema Kim ameamua dhidi ya ndoa yake na Kanye na anajitayarisha kwa talaka, lakini bado anabidi kuwakilisha hati za kukamilisha jambo hilo.

⚫️ Kwa UPDATES zote, Download GLOBAL APP: ⚫️ ANDROID:http://bit.ly/38Lluc8 ⚫️ iOS:https://apple.co/38HjiCx

⚫️ Kwa UPDATES zote, Download GLOBAL APP: ⚫️ ANDROID:http://bit.ly/38Lluc8 ⚫️ iOS:https://apple.co/38HjiCx

Leave A Reply