Mkuu wa Majeshi Malawi Kushiriki Johnnie Walker Waitara Golf

Mkuu wa Majeshi ya Malawi, Jenerali Vincent Thom Nundwe, akijiandaa kupiga mpira katika mashindano ya Johnnie Walker Waitara Golf Trophy yanayodhaminiwa na Kampuni ya Bia ya Serengeti kupitia kinywaji cha Johnnie Walker ikiwa ni sehemu ya kuisapoti michezo nchini. Mashindano hayo yamefanyika katika Viwanja vya Lugalo Golf Club jijini Dar es Salaam leo.

MKUU wa Majeshi ya Malawi, Jenerali Vincent Thom Nundwe anatarajiwa kushuhudia na kushiriki mashindano ya Johnnie Walker Golf Waitara Trophy  yanayotarajiwa kufanyika kesho Januari 23, 2021 katika Viwanja vya Lugalo Golf Club, Dar es Salaam.

Katika mashindano ya leo yaliyowakutanisha wachezaji wa kulipwa ambao wamecheza viwanja 18, Professional kutoka Lugalo Golf Club, Bryson Nyenze ameibuka na ushindi.

Mashindano hayo yanadhaminiwa na kinywaji cha Johnnie Walker (JW) kinachosambazwa na Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL). Johnnie Walker ni moja kati pombe kali zenye ubora wa hali ya juu na hadhi ya kimataifa.

Kinywaji hiki kina jumla ya aina tano ambazo zimeshinda tuzo za ubora wa kimataifa. Aina hizo ni pamoja na JW Red Label, JW Black Label, JW Green Label, JW Gold Label, na JW Blue Label kila moja ikiwa na historia yake ya kipekee.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia ya Serengeti, Mark Ocitti akipiga mpira katika mashindano ya Johnnie Walker Waitara Golf Trophy yanayodhaminiwa na Kampuni ya Bia ya Serengeti kupitia kinywaji cha Johnnie Walker ikiwa ni sehemu ya kuisapoti michezo nchini.

Akizungumzia maandalizi ya mashindano ya kesho, Afisa Habari wa Lugalo Golf Club, Kapteni Selemani Semunyu amesema maandalizi yamekamilika na mashindano yataanza saa moja asubuhi hadi saa 10 jioni kisha zoezi la utoaji zawadi litafuatia.

“Kama mjuavyo kwenye mchezo wa Golf kwa wachezaji wa ridhaa zawadi huwa ni vitu, kwa hiyo vitu venye thamani kesho wataviona. Kwa wachezaji wa kulipwa zawadi huwa ni fedha, nina matumaini kiwango halisi kesho tutakitangaza wakati zoezi zima la ugawaji wa zawadi,” amesema Kapteni Semunyu.

Pia amechukua fursa hiyo kuwataka mashabiki kujitokeza kwa wingi kutazama mashindano hayo ambayo  yatakutanisha wachezaji 150. Amesema kila wakati wamekuwa wakiwaita mashabiki kwa kuwa Golf ni kama mchezo mwingine, hivyo mashabiki wanaruhusiwa kuangalia mchezo huo.

Toa comment