The House of Favourite Newspapers

Kim Poulsen: Hii Taifa Stars Ni Tamu Balaa

0

KOCHA Mkuu wa Taifa Stars, Kim Poulsen, amesema kuwa Watanzania wanatakiwa kuelewa kuwa wana timu bora sana ya taifa kwa sasa na wanatakiwa kuwa na imani nayo na kutoa sapoti kubwa.

 

Kim aliyasema hayo baada ya Stars kuinyuka Afrika ya Kati mabao 3-1 kwenye mchezo wa kimataifa wa kirafiki uliopo kwenye kalenda ya Fifa uliochezwa Uwanja wa Mkapa, Dar, ukiwa ni mchezo wa kwanza kati ya mitatu ambayo watacheza.

 

Akizungumza na Championi Ijumaa, Kim alisema Tanzania ina timu bora sana ya taifa ambayo inaweza kufanya vizuri kwenye mchezo wowote wa kimataifa na jambo ambalo Watanzania na wapenda soka nchini kote wanatakiwa kutoa sapoti ya kutosha kwenye kila mchezo ambao timu hiyo itacheza kwa sasa.

“Nilizungumza kabla ya mchezo kuwa tuna timu bora sana ya taifa, wachezaji bora pengine kuliko nyakati za hivi karibuni, hatukuwahi kuwa nao kwa wakati mmoja.

 

“Tuna timu ambayo inaweza ikashindana kwenye mchezo wowote wa kimataifa na ikafanya vizuri. Watanzania na wapenda soka wote wanapaswa kuisapoti timu yetu,” alisema Kim.

 

Stars inajiandaa na michezo ya kufuzu Afcon 2023 ambapo itaanza michezo yake Juni, mwaka huu.

STORI NA ISSA LIPONDA, CHAMPIONI IJUMAA

YANGA WATUA kwa AZIZ KI wa ASEC MIMOSAS, INJINIA Afunguka KILA KITU | KROSI DONGO..

 

Leave A Reply