The House of Favourite Newspapers

Kimbunga Eunice Chasababisha Maafa Makubwa Uingereza

0

TAKRIBANI watu wanne wamefariki dunia huku nyumba takribani 435,000 na mali nyingine yakiwemo magari, zikiharibiwa vibaya kufuatia Kimbunga Eunice kilichoipiga Uingereza hapo jana Ijumaa, Februari 18, 2022, kikiwa na kasi ya inayokadiriwa kufikia 122MPH.

 

Zaidi ya nyumba milioni 1.1 ziliachwa bila umeme kufuatia kimbunga hicho kuharibu vibaya gridi ya taifa ya umeme nchini humo ambapo mpaka sasa, hasara iliyosababishwa na kimbunga hicho inakadiriwa kufikia Paundi milioni 360 za Uingereza.

 

Kasi ya kimbunga hicho, inatajwa kuwa kubwa na iliyovunja rekodi, tangu mwaka 1987 Uingereza ilipopigwa na kimbunga kingine kikubwa cha Great Storm.

Leave A Reply