The House of Favourite Newspapers

Kimei Aiteka Vunjo, Moshi.

0

Aliyekuwa Mkurugenzi Mtendajiwa Benki ya CRDB, Dkt. Charles Kimei ambaye sasa ni mteule wa Chama cha Mapinduzi (CCM) katika Ubunge wa Jimbo la Vunjo, mkoani Kilimanjaro, leo amevunja rekodi kwa umati mkubwa uliojitokeza kumsindikiza kurudisha fomu katika ofisi za tume ya uchaguzi mjini Moshi.

Msafara mrefu uliojumuisha magari, Daladala, Bodaboda na Baiskeli ulimuongoza mgombea huyo aliyekuwa kwenye gari la wazi kutoka nyumbani kwake kijini Mamba, Marangu mpaka kwenye ofisi za tume hiyo katikati ya mji wa Moshi.

Mmoja wasindikizaji aliyejitambulisha kwa jina la Enos Makundi alisema kuwa ni mara ya kwanza kwa historia ya Jimbo la Vunjo, ambalo kwa muda mrefu limekuwa chini ya upinzani kumpokea mwana CCM kwa kishindo kikubwa hivyo.

“Kimei ameleta sura mpya katika siasa za Vunjo mara nyingi mapokezi haya walipewa wapinzani lakini ujio wa Kimei ambaye ni mzawa wa hapa mwenye kukubalika na wengi, umeleta hamasa.

Tunamuaminia sana” alisema.

Akizungumza baada ya kukabidhi fomu kwa Tume ya Uchaguzi mjini Moshi, Dokta Kimei ambaye ni mchumi mbobevu, alisema kuwa imani kubwa iliyopo kwa Raisi Magufuli, Chama cha Mapinduzi pamoja na yeye kama mgombea vimewapa matumaini mapya wanavunjo.

Nakishukuru sana Chama changu cha Mapinduzi (CCM), chini ya Mwenyekiti Dokta John Pombe Magufuli, kwa kuniamini, na kunipa nafasi ya kugombea kuwawakilisha wanavunjo.

Hii ni heshima kubwa sana kwangu Nawasihi wana Vunjo wote tuungane kwa maslahi mapana ya jimbo letu la Vunjo ili tulete maendeleo kwa kizazi kilichopo na kijacho.

Leo napenda kuanza na shukrani kwa kila mtu aliyewezesha kuanza safari hii.

Siku chache zijazo nitaeleza kwa undani mpango mkakati wangu, ambao naamini kwa kushirikiana na kila mwenye kuitakia mema Vunjo, tafanikiwa.

Pamoja Tunaweza” alisema msomi huyo aliyezaliwa na kukulia katika Kijiji cha Komakundi, Kata Mamba, Marangu.

Leave A Reply