The House of Favourite Newspapers

Kimenuka! Ali Kiba Aburuzwa Mahakamani

MWANAMKE mfanyabiashara wa nguo za mitumba, Hadija Hassan amefungua kesi ya madai ya matunzo ya mtoto dhidi ya Staa wa Bongo Fleva, Ali Saleh Kiba ‘Ali Kiba’ akidai jumla ya Sh. milioni 1.41, ikiwemo Sh. 950,000 za ada na Sh. 460,000 za matumizi ya mtoto wa miaka mitano (jina limehifadhiwa kwa sababu za kisheria na kimaadili).
Hadija amefungua kesi ya madai hayo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam akidai matunzo kwa mlalamikiwa ambaye ni mzazi mwenziye, King Kiba ambapo mujibu wa hati ya madai iliyowasilishwa mahakamani hapo, mlalamikaji anadai kuwa Januari, 2013 katika Hospitali ya Mikocheni, Dar alizaa mtoto wa kike ambaye baba yake ni mlalamikiwa.
Alidai kupitia hati hiyo kwamba mlalamikiwa anatakiwa kumhudumia mtoto huyo kwa mahitaji yote muhimu ikiwamo chakula, nguo, elimu na matibabu.
“Kutokana na Sheria ya Watoto ya mwaka 2009, mdaiwa anatakiwa kutoa huduma kila mwezi, chakula Sh. 150,000, matunda Sh. 50,000, chakula cha ziada Sh. 50,000, michezo na burudani za watoto Sh. 100,000, nguo Sh. 60,000 na matibabu Sh. 50,000 ambapo jumla ni Sh. 460,000,” alidai mlalamikaji kupitia hati hiyo.

Katika madai haoyo, mlalamikiwa anatakiwa kumlipia mtoto ada ya shule kwa muhula Sh. 950,000, na anadaiwa aliacha kutoa matunzo hayo tangu Januari, 2018 hivyo anaiomba mahakama imwamuru mdaiwa kutoa matunzo hayo ya Sh. 460,000 kila mwezi na ada.
Mlalamikaji anaomba malipo ya kwanza yatolewe mapema baada ya hukumu, na pia anaiomba mahakama imwamuru King Kiba kumsomesha mtoto, kumnunulia nguo na matibabu ikiwamo kumtafutia bima ya afya, kulipa gharama za matunzo Sh. 460,000 kuanzia Februari 2017 mpaka siku itakapotolewa hukumu na gharama za kesi ziwe kwa mdaiwa, mahakama itoe amri nyingine yoyote itakayoona inafaa kwa manufaa yake. Kesi imefunguliwa kwa msaada wa Kituo cha Wanawake cha Msaada wa Kisheria (WLAC).

Sarah wa Harmonize na Mwarabu Fighter ni Wapenzi?

Comments are closed.