The House of Favourite Newspapers

JPM AWAONYA SUA DHIDI YA KUFANYA FUJO, SIASA – VIDEO

RAIS  John Magufuli amesema haiwezekani kwa watoto wa viongozi wenye nyadhifa za juu nchini akiwemo mtoto wake na wa wakuu wa mikoa wakajaza fomu kuomba mikopo katika Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (Heslb).

 

Hayo ameyasema leo wakati akihutubia kwenye hafla alipotembelea Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) kilichopo mkoani Morogoro na kutoa onyo kwa wanafunzi wa vyuo vyote nchini wasijihusishe na makundi ambayo yanaweza kuwashawishi wakajiingiza katika migomo na fujo zisizokuwa za lazima ambazo zinaweza kugharimu maisha yao na kufuta ndoto zao za kielimu.

 

“Ukweli lazima niwaeleze, haiwezekani na haiingii akilini eti umchukue mtoto wangu au wa mkuu wa mkoa naye apewe mkopo, haiwezekani, kila kitu lazima kiende kwa mipangilio, vyanzo vyetu vya mapato ni vichache. Shule ya msingi umesoma private school, secondary nayo, private school, leo unakuja kuchukua fomu ujaze ili wakupe mkopo, wamekuwa vichaa?

 

“Ninyi mmekuja hapa kwa ajili ya kupiga shule, msipoteze muda wenu kwa mambo yasiyo na tija. Serikali imetoa mikopo kwa wanafunzi 6,000, pigeni shule, msigeuze vyuo kuwa sehemu za siasa. Kila mmoja wenu ana maisha yake na baba yake na mama yake.

 

“Ninyi ndiyo taifa la leo, kesho na kesho kutwa, kama kutatokea chuo chochote kikafanya fujo, wala sitasita kufukuza, nikishawafukuza sijui nitawarudisha lini,” alisema Rais Magufuli.

MSIKIE RAIS MAGUFULI AKIFUNGUKA HAPA

Comments are closed.