The House of Favourite Newspapers

KIMENUKA! POGBA ATIFUANA NA MOURINHO MAZOEZINI – VIDEO

MCHEZAJI wa klabu ya Manchster United, Paul Pogba na kocha wake, Jose Mourinho, wameonekana katika mkanda wa video wakibadilishana maneno makali  wakati wa mazoezi asubuhi ya leo.

 

Wakati huohuo, Mourinho amethibitisha kwamba amemnyang’anya unaibu nahodha mchezaji huyo baada ya timu hiyo kushindwa katika mchezo wake dhidi ya Derby katika mpambano wa Kombe la Carabao jana.

 

Shirika la utangazaji la Sky Sport News ambalo lilikuwepo kwenye mazoezi hayo asubuhi hii, limesema kwamba matukio hayo yamezidi kuvuruga uhusiano baina ya watu hao wawili.

 

Katika mkanda uliopigwa hapo, Pogba anaonekana akifanya mazoezi ya kukimbia kuelekea kwa kocha msaidizi, Michael Carrick, Mourinho na ofisa wa idara ya habari ya klabu hiyo. Mara mchezaji huyo anashikana mikono na kila mmoja wa watu hao na kisha Mourinho anawambia kitu fulani Pogba ambaye anaonekana kukasirika.

 

Wawili hao wanaendelea kulumbana wakati Mourinho anaendelea kuzungumza huku akiondoka kuelekea waliko wachezaji wengine mazoezini. Yote haya yanafanyika pia mbele ya maofisa wa klabu hiyo, Ricardo Formosinho na Carlos Lalin.

 

Hata hivyo, baada ya malumbano hayo, Mourinho anasema: “Uamuzi wa kumwondoa Pogba katika nafasi ya unaibu nahoba haukutokana na sababu yoyote.  Hapakuwa na tatizo.  Mtu anayeamua kumwondoa mtu katika unaibu nahodha ni yuleyule aliyempa nafasi hiyo, mimi mwenyewe.

“Mimi ndiye meneja na kocha wake.  Hakuna kutoelewana au tatizo lolote isipokuwa moja tu, ambalo sitaki kulieleza.”

VIDEO: TAZAMA VIDEO YA TUKIO HAPA

Comments are closed.