The House of Favourite Newspapers

SIMULIZI YA MAHABA: KANDAMBILI HAIPIGWI KIWI

KAMA nakuona vile shoga yangu ulivyotumbua macho kuangalia kaniki ikiwekewa dawa ya madoa! Heee heeeeiyaaaaaa! Na utashanga’ sana mwaka huu wakati unajua kabisa thamani ya kopo la chooni hadhi yake chooni kabatini likafuate nini?  

 

Kama ulikuwa hujui jua sasa, maisha ni vitendo na ukishatendwa ndiyo utajifunza, upo nyonyo? Siyo unazubaazubaa mwenzangu na mimi kumbe una nyota ya mihogo ya kukaangwa kutwa kupendwa na wanafunzi, haloooo eeeehhh!

 

Si unanijua tena Anti mimi nikishaanza hii kona yetu ya kujidaidai lazima nikupe udambwiudambwi wa kutosha, upo? Wajanja wa mjini wanakwambia pesa ni elfu kumi tu hizo nyingine zote ni chenji! Weeeeeeraaaaa! Shoga hakuna kitu kinachokera kama kumuona mumeo hafai, nimekuwa nikipata meseji nyingi za wasomaji wanalalamikia tu waume zao mara ohhh hawawaridhishi, mara ohhh wanene sana na wana vibamia! Haohao ukiwauliza umeolewa naye anakujibu ndiyo, una watoto naye anakujibu ndiyo, shuuuutuuuuu usiye na haya!

 

Tena uwaambie na wenzako ambao wao wanajiona kama wana nyota ya paka kupendwa na wachawi, mwanaume hachaguliwi na kukuridhisha wewe inategemea ni watundu kiasi gani! Mwanaume hata awe bonge au na kibamia vipi kama wewe ni mtundu uliyefunzwa unyagoni ukafunzika unaweza kuridhishwa naye, upo nyonyo?

 

Kuna mashosti wengine wanajifanya kuwachukia wanaume wanene kwa madai kuwa hawawezi shughuli faragha, komaaaa! Tangu lini kandambili zikapigwa kiwi? Aliyekwambia ukiwa mnene huwezi kila kitu nani? Wee kaakaa tu, endelea kuchagua wa kukuoa na kuishi naye halafu ujidanganye kwenye akili yako kuwa mwanaume mnene ni wa kumlia vyake na kusepa lakini si wa kuolewa naye uone wenzako wanavyopita naye!

 

Siku hizi shoga, mwenye bomba hakai foleni, ukiona hakufai mwenzako anamfaa ati! Najua wengine kama bata tu, hata umpe kokoto kiasi gani ataharisha tuuuuuu, heee eheeeeeiyaaaaa! Ukiona kuku yupo kwa mganga ujue rangi yake ndiyo imemponza, nicheke miye nitanue mbavu zangu baadaye!

 

Nikugeukie na wewe mwembamba unayewachukia wanaume wanene na wao wangekuchukia kwa wembamba wako unafikiri duniani tungeishi hapa? Au ndiyo tungeishi wote wembamba! Labda nikung’ate tu sikio shoga yangu, mwanaume au mwanamke mnene haangaliwi kwa umbo bali shughuli yake! Anaweza kuwa mnene kwa kila kitu lakini mkifika faragha anamzidi hata yule mwembamba, shughuli yake tu japo ndiyo unamuona kibamia mbona utajuuutaaa!

 

Kwa leo shoga naomba niishie hapa nisije kuwa mbeya kama kwapa, kuvuja jasho mpaka ubebe mzigo! Kwa ushauri nitumie meseji tu kwenye namba yangu hapo juu nitakusaidia.

Ni mimi Shangingi Mstaafu Anti Naa ukipenda niite Anti Nasra.

Comments are closed.