The House of Favourite Newspapers

‘Kinachomtesa Chid ni hiki!’

0
Chid Benz.

MTAALAM wa saikolojia, Mkang’u Lyadunda amesema kinachomtesa staa wa Hip Hop, Rashid Makwiro ‘Chid Benz’ ni kutopata tiba sahihi baada ya kutoka ‘sober house’.

Lyadunda aliiambia Over Ze Weekend kuwa, mkali huyo amejikuta akirudia kwenye matumizi ya madawa ya kulevya kwa sababu wanaomzunguka hawajaelekezwa namna ya kuishi naye, kuhudhuria mikutano mbalimbali ya wanasaikolojia.

“Madawa ya kulevya ni kama vile magonjwa ya kisukari, yakiingia ni ngumu kutoka moja kwa moja.

“Watu wanaomzunguka Chid Benz wanapaswa kuishi naye kwa kufuata maelekezo ya wanasaikolojia na ahudhurie mikutano mbalimbali ya kumjenga kisaikolojia, vinginevyo ni ngumu kuacha hata kama amemaliza tiba ya sober,” alisema Lyadunda.

 OVER ZE WEEKEND | IJUMAA WIKIENDA

Shuhudia Uzinduzi Rasmi wa Kihistoria wa Sokabet (Video)

Leave A Reply