The House of Favourite Newspapers

SITASAHAU NILIPOLALA NA MWANAMKE JUU YA KABURI (18)

0

SITASAHAU NILIPOLALA NA MWANAMKE JUU YA KABURI (18)

 

ILIPOISHIA…

Nakumbuka siku moja niliamua kwenda kanisani kufanyiwa maombi ya tatizo langu hili. Nilipokuwa njiani kueleka huko, mtu wa ajabu akatokea akiwa na hasira kuliko siku zote nilizowahi kumshuhudia. Siku hiyo alinikimbiza mpaka akanikamata, kisha akanikata kidogo mguu wangu kwa upanga wake na kusababisha damu kiasi ichuruzike. Toka siku hiyo, sikurudia tena njia hii.

 

ENDELEA KUISOMA…

Asubuhi ya siku ya Jumamosi, ‘nilitupia’ shati la kaki na suruali nyeusi kisha chini nikavalia buti kubwa nyeusi nilizopewa na rafiki yangu mwanajeshi. Siku hiyo niliamua kwenda ufukweni kupumzisha akili kutokana na mikikimikiki ya kukimbizwa na maisha na kufukuzwa na mtu wa kutisha. Zimwi likujualo halikuli likakwisha, mtu wa ajabu alinitafuna taratibu na punde ningebaki mifupa!

 

Nilifika ufukweni. Mandhari yake yalipendeza. Kwa muda nikayasahau yale masahibu yangu ya siku zote. Katika jambo ambalo nilifurahi kuliona, ulikuwa ni ule ugonjwa wangu wa miaka mingi ulionipa mkasa wa kufukuzwa muda wote. Wanawake.

 

Walikuwako wengi. Nao kwa uchokozi walivalia nguo za ndani tu. wengi wakijitia kuogelea kama samaki. Wizi mtupu!… BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI

Leave A Reply