The House of Favourite Newspapers

Kinda Man City Adaiwa Kujiua Baada ya Kuachwa

0

 

KINDA wa Man City, Jeremy Wisten (17),  inadaiwa kuwa amejiua kutokana na msongo wa mawazo baada ya kuachwa na  klabu hiyo.

 

Jeremy ni mzaliwa wa Malawi ambaye alihamia England na familia yake wakati akiwa bado mdogo na baadaye kuanza maisha yake soka akiwa na Juniors FC na 2014 akajiunga na De la Salle FC.

 

Mwaka 2016  alisajiliwa na Man City katika kikosi cha U-13 na kuanza safari yake ya soka ambapo hakupata nafasi timu ya wakubwa, hata hivyo,  vyanzo vya baadhi vinaripoti kuwa mchezaji huyo kajiua huku wengine wakiripoti kifo chake pasipo kutaja sababu.

Leave A Reply