The House of Favourite Newspapers

KINGDOM JUICE WATEMBELEA GLOBAL PUBLISHERS

Mabalozi wa Kingdom Juice wakisoma magazeti ya Amani ndani ya eneo la wageni katika kitengo cha magazeti Pendwa.

MKURUGENZI wa Kingdom Juice, Zabron Julius,  akiwa na mabalozi wa juisi hizo, Clavery and Kelv, mapacha wanaojiita One Face, wametembelea Kampuni ya Global Publisher, Sinza-Mori jijini Dar na kujionea shughuli mbalimbali za uzalishaji wa magazeti ya Ijumaa Wikienda, Uwazi, Risasi, Amani, Ijumaa, Risasi Jumamosi, Championi na Spoti Xtra.

Wakiwa Global, walitembelea vitengo mbalimbali ikiwemo Global TV pamoja na dawati la IT ambapo walizungumza na wahariri pamoja na baadhi ya waandishi wa habari ambapo Zabron alisema wanatumia fursa ya kufika Global kubadilishana mawazo na waandishi lakini pia kutangaza juisi zao ambazo zinapatika maeneo mbalimbali jijini Dar.

Mabalozi wa Kingdom Juice na mkurugenzi wao wakisalimiana na Mhariri Kiongozi wa Magazeti Pendwa, Amran Kaima (kushoto).

“Juisi zetu ni nzuri, hazina kemikali yoyote kwani zinatengenezwa kwa matunda halisi. Niwasihi Watanzania wazijaribu juisi zetu,  tunapatikana Afrika Sana, Mikocheni na pia tupo  Tabata-Segerea pale Stand,” alisema Zabron.

Matukio katika Picha

Kingdom Juice wakiwa na waandishi wa Magazeti Pendwa.

Mabalozi wa Kingdom Juice, Clavery And Kelv,  wakiwa ndani ya Studio za Global TV.

PICHA/HABARI: ERICK EVARIST/GPL

Comments are closed.