The House of Favourite Newspapers

BREAKING NEWS: WEMA AKANA KOSA, AACHIWA KWA DHAMANA

MSANII wa filamu nchini, Wema Sepetu,  leo Novemba 1, 2018 amepandishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na shtaka la kusambaza video  ya ngono kupitia mtandao wa kijamii wa Instagram.

Wema amesomewa shtaka hilo mbele ya Hakimu Mahira Kasonde ambapo amekana kosa hilo kisha kuachiwa kwa dhamana ya Sh. milioni 10 kupitia kwa Salim Limu.

 

Aidha, Wema ambaye alikuwa akiwakilishwa na wakili  Reuben Simwanza, ametakiwa asiposti video au picha yoyote isiyo na maadili au inayoashiria ngono kwenye mitandao.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Novemba 20, mwaka huu.

 

Akizungumza baada ya kesi hiyo kuahirishwa, Mkurugenzi wa Huduma za Sheria wa  Mamlaka ya Kudhibiti Mawasiliano nchini (TCRA) Johannes Karungura amesema:
“TCRA tupo makini, tunapenda kuwatahadharisha wale wote waliokuwa na picha na video za namna hiyo wazifute katika simu zao, kwa sababu haziruhusiwi.”

Comments are closed.