The House of Favourite Newspapers

Kinyambe kuzikwa kesho, jina lake lazua utata

0

AvOo-VWKi6Wl9LQq8vhzmEAs2J1yd736rmzxzMImCRvVMarehemu James Peter a.k.a Kinyambe

Na Ojuku Abraham
MSANII wa vichekesho James Peter Nsemwa maarufu kama Kinyambe ambaye alifariki dunia jana mkoani Mbeya, atazikwa kesho katika makaburi ya Uyole mkoani Mbeya.

https://www.youtube.com/watch?v=GoRF5jOx4S8

Baba wa marehemu, mzee Lugendelo Nsemwa, ameuambia mtandao huu akiwa nyumbani kwake Uyole, kuwa mwanaye ambaye alijipatia umaarufu mkubwa kutokana na uwezo wake wa uchekeshaji, alianza kuumwa tangu Juni mwaka jana, ambapo tumbo na miguu ilikuwa imejaa maji. Alisema tatizo hilo lilipelekea mapafu yake kushindwa kufanya kazi sawasawa.

“Kwa kipindi kirefu alikuwa amelazwa katika hospitali binafsi ya Abaja iliyopo Uyole, lakini Mei 9 mwaka huu, hali yake ilibadilika, alizidiwa na kupoteza fahamu, kitu kilichofanya tumkimbize katika hospitali ya mkoa wa Mbeya iliyopo maeneo ya Forest ya zamani, ambako alilazwa katika wodi ya ‘private’ chumba namba 4, na bahati mbaya jana (Jumatano) saa 3.5 akafariki dunia,” alisema mzazi huyo.

Kinyambe2

Kinyambe (kulia) akiwa na msanii mwenzake Masai Nyota Mbofu enzi za uhai wake.

Katika hali ya kushangaza, mzazi huyo alisema jina la Mohamed Abdalah, ambalo linafahamika kwa wengi kama ndilo halisi la msanii huyo, yeye halitambui, kwani tangu amezaliwa alipewa jina hilo na hakuwahi kusikia kama alilibadili.

Aidha, aliwalaumu wasanii wenzake kwa kutotoa msaada wowote wakati wa ugonjwa, kwani kwa kipindi chote hakuwahi kuwaona wasanii wa Dar es Salaam wala kupata salamu zao, zaidi ya kuwaona wale wa Mbeya ambao nao walikuwa wakienda mara mojamoja.

KINYAMBEAkionyesha manjonjo enzi za uhai wake.

Daktari mmoja wa hospitali hiyo aliyemhudumia marehemu tangu alipolazwa, ambaye jina lake linahifadhiwa kwa kuwa siyo msemaji wa hospitali hiyo, alisema marehemu alipopokelewa na kupimwa, aligundulika kupungua kwa kiwango cha sukari mwilini huku pia akiwa na homa ya mapafu.

https://www.youtube.com/watch?v=vzdULm-sDM8

Wakati wa uhai wake, Kinyambe aliwahi kuishi na wanawake watatu, ambao majina yao hayakuweza kupatikana mara moja, lakini imefahamika kuwa wa kwanza alizaa naye mtoto mmoja, wa pili alizaa naye mtoto mmoja pia, lakini alifariki mwezi uliopita akiwa na miaka mine. Mwanamke wake wa mwisho, ni mjamzito ambaye endapo Mungu atamjaalia, atajifungua mwezi ujao.

Marehemu alijipatia umaarufu kwa vichekesho vyake kupitia vipindi mbalimbali vya televisheni, kikiwemo cha Vituko Show katika Channel Ten na pia aliwahi kufanya kazi na Sharo Milionea.
Mungu Ilaze Roho ya Marehemu Mahali Pema!

Leave A Reply