The House of Favourite Newspapers

Kiongozi wa Hamas Athibitisha wanawe watatu wa kiume kuuawa katika shambulio la anga

0
Kiongozi mkuu wa Hamas Ismail Haniyeh

Kiongozi wa kisiasa wa Hamas Ismail Haniyeh amethibitisha kuwa wanawe watatu na wajukuu zake wanne waliuawa katika shambulio la anga huko Gaza.

Vyombo vya habari vinavyohusishwa na Hamas vilisema gari walilokuwa wakisafiria wanawe lilishambuliwa katika kambi ya Al-Shati karibu na mji wa Gaza.

Haniyeh alisema kuwa tukio hilo halitabadilisha matakwa ya Hamas katika mazungumzo yanayolenga kufikia makubaliano ya kusitisha mapigano.

Wanajeshi wa Israel walisema vijana hao walikuwa wanachama wa tawi la kijeshi la Hamas.

Kundi hilo liliripotiwa kwamba lilikuwa likielekea kwenye sherehe ya familia kuadhimisha siku ya kwanza ya sikukuu ya Eid ya Waislamu.

Jeshi la Israel limewataja ndugu hao watatu, mmoja kama kamanda na wawili kama maafisa wa kijeshi.

Leave A Reply