The House of Favourite Newspapers

Mafuriko Makubwa ya mvua Yatokea Arusha Usiku wa Kuamkia Leo, Yasomba vitu mbalimbali – Video

0

MAFURIKO makubwa ya mvua yametokea mkoani Arusha usiku wa kuamkia leo Alhamisi Aprili 11, 2024 ambayo yanasomba vitu mbalimbali ikiwemo magari ya watu na kuhatarisha maisha ya wananchi.

Vyanzo vya awali vinadai mafuriko hayo ni matokeo ya mvua zinazoendelea kunyesha maeneo mbalimbali ya nchini ikiwemo Arusha.

Mpaka sasa hakuna taarifa rasmi iliyotolewa na mamlaka ya Serikali juu ya mafuriko hayo na athari ambazo zimejitokeza ingawa katika eneo la Kisongo nje kidogo ya jiji la Arusha hali inaenokana kuwa mbaya zaidi.

Leave A Reply