Kipa Mpya Yanga SC Azidiwa Uwezo na Kabwili

KOCHA wa Makipa Yanga, Razack Siwa amefunguka kuwa kinachomzuia kipa wake, Erick Johora kucheza tangu kuanza kwa msimu huu ni ushindani mkubwa anaopata kutoka kwa makipa wenzake ambao ni Djigui Diarra na Ramadhan Kabwili.

 

Johora tangu asajiliwe Yanga kwenye dirisha kubwa la usajili hajawahi kucheza mchezo wowote wa ligi pamoja na ile ya Ligi ya Mabingwa pia ule wa Ngao ya Jamii dhidi ya Simba.

 

Akizungumza na Championi Jumatano, Siwa alisema kuwa: “Nafikiri wote ni makipa wazuri sana kusema ukweli ila nadhani ni changamoto na ushindani mkubwa uliopo ndio maana kila mmoja anataka kupambana ili atimize malengo yake.

 

“Nafasi ya kipa ni moja tu uwanjani tofauti na maeneo mengine kama mabeki, viungo na hata washambuliaji kwa hiyo unapopata nafasi unatakiwa upambane sana na uitendee vema ili anapokuja mwingine aweze kupambana zaidi yako.

 

“Johora hajapata nafasi tu kwenye kikosi ila ni kipa mzuri sana nina imani akipata nafasi anaweza kuonyesha kitu na akapata nafasi kwenye timu kama hao wengine wanavyopata nafasi,“ alisema Siwa.

Leen Essau, Dar es Salaam


Toa comment