The House of Favourite Newspapers

Kipa Simba: Hans Poppe msajili Sangare haraka

0

zacharia-hans-poppe_n360ocbduj881lruz5fbf18hqZacharia Hans Popp

Said Ally na Omary Mdose

MLINDA mlango wa Simba, Vincent Angban raia wa Ivory Coast, amefunguka kuwa endapo usajili wa Morisane Sangare raia wa Ivory Coast utakamilika, basi timu hiyo itakuwa imelamba dume kwani jamaa ni ‘mtu wa kazi’ si kitoto.

Kamati ya Usajili ya Simba inayoongozwa na mwenyekiti wake, Zacharia Hans Poppe ipo katika mikakati ya kukijenga kikosi hicho kwa msimu ujao kwa kuanza kusajili wachezaji ambapo jina la Muivory Coast huyo lipo katika orodha ya wale watakaokuja kufanya majaribio kabla ya kusajiliwa.

Angban ameliambia Championi Jumatano, kuwa anaufahamu vyema uwezo wa Sangare kwani amecheza naye nchini kwao, hivyo kuwataka viongozi kufanya kila liwezekanalo kuhakikisha wanampata kumjua kuwa mtu wa shughuli.

 “Ni mchezaji mzuri, nimecheza naye Asec Mimosa, si kwamba namsifia, muulize hata Wawa (Pascal beki wa Azam) anamjua vizuri kwani tulicheza wote tulipokuwa Ivory Coast.

“Endapo usajili wake ukikamilika basi naona kuwa Simba itakuwa imepata mtu sahihi ambaye kwa uwezo wake na sisi tuliopo naona kuwa tutapata mafanikio kwani najua vyema kiwango chake,”alisema Angban.

KUNUNUA NA KUSOMA MAGAZETI YA GLOBAL PUBLISHERS ONLINE, INGIA HAPA==>VODACOM M-PAPER APP

*********

JIUNGE NA SOCIAL MEDIA ZETU:

KWA HABARI ZA KITAIFA, KIMATAIFA, MASTAA NA MIKASA YA KUSISIMUA

INSTAGRAM: @Globalpublishers

ERIC SHIGONGO INSTAGRAM: @ericshigongo

TWITTER: @GlobalHabari

FACEBOOK: @GlobalPublishers

SUBSCRIBE YOU TUBE: GlobalPublishers

GLOBAL TV ONLINE: www.globaltvtz.com

HADITHI ZA KUSISIMUA NA MBINU ZA UJASIRIAMALI, ERIC SHIGONGO FACEBOOK PAGE: @shigongotz

Leave A Reply