The House of Favourite Newspapers

Pluijm ambeba kiungo mpya CAF

0

pluijm1Kocha Mkuu wa Yanga, Hans van Der Pluijm.

Nicodemus Jonas, Dar es Salaam

NI kama Kocha wa Yanga, Hans van Der Pluijm ana uhakika wa kutinga hatua ya makundi leo kwa kuwaondoa Waangola, Sagrada Esperanca katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika, hii ni baada ya kumuamuru kiungo wake mpya,  Juma Mahadhi ‘Kiberenge’  kujifua kivyake huko Tanga kwa kile alichomwambia anatarajia kumtumia katika michezo ijayo.

Yanga inaingia uwanjani leo Jumatano ikiwa na faida ya ushindi wa mabao 2-0 walioupata katika mchezo wa awali uliopigwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar na iwapo itafuzu, basi inaruhusiwa kuongeza wachezaji wengine na jina la kwanza kuhakikishiwa nafasi hiyo ni Mahadhi aliyesaini miaka miwili akitokea Coastal Union na Hassan Kessy kutoka Simba.

Kiungo huyo ameliambia Championi Jumatano kuwa, tayari ameanza kutekeleza agizo la Pluijm kwa programu ya kusaka pumzi na stamina.

“Unajua baada ya kusaini, nilirejea Tanga lakini juzikati nilipata simu ya viongozi wa Yanga wakaniambia kocha amesema niendelee kujifua kwa ajili ya michuano ya kimataifa, kwamba kama watafuzu atanitumia. Naendelea na mazoezi binafsi na kikubwa ni mazoezi ya pumzi na stamina,” alisema kiungo huyo ambaye pia anaweza kucheza kama fowadi.

KUNUNUA NA KUSOMA MAGAZETI YA GLOBAL PUBLISHERS ONLINE, INGIA HAPA==>VODACOM M-PAPER APP

*********

JIUNGE NA SOCIAL MEDIA ZETU:

KWA HABARI ZA KITAIFA, KIMATAIFA, MASTAA NA MIKASA YA KUSISIMUA

INSTAGRAM: @Globalpublishers

ERIC SHIGONGO INSTAGRAM: @ericshigongo

TWITTER: @GlobalHabari

FACEBOOK: @GlobalPublishers

SUBSCRIBE YOU TUBE: GlobalPublishers

GLOBAL TV ONLINE: www.globaltvtz.com

HADITHI ZA KUSISIMUA NA MBINU ZA UJASIRIAMALI, ERIC SHIGONGO FACEBOOK PAGE: @shigongotz

Leave A Reply