The House of Favourite Newspapers

‘Jahazi’ Chafungiwa, Vituo 3 vya Redio Vyaonywa

0

KAMATI ya Maudhui ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imekifungia kipindi cha Jahazi kinachorushwa na redio ya Clouds FM kuanzia leo Ijumaa tarehe 14 Agosti 2020 kutokana na kosa la kuhamasisha kitendo cha kujichua.

Pia, kamati hiyo imeviweka chini ya uangalizi wa miezi mitatu vituo vya radio vya Radio One na RFA huku Abood FM ikiwekwa chini ya uangalizi miezi sita kwa kosa la kurusha mahojiano ya Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Bara, Tundu Lissu bila kuzingatia mizania ya habari.

Kamati hiyo, imetahadharisha kuwa hatua kali zitachukuliwa dhidi ya vituo hivyo iwapo havitajirekebisha ndani ya muda huo.

 

Wasafi Media Online TV imetuhumiwa kurusha maudhui yanayochochea vitendo vya ngono kupitia kipindi cha Women Matters. Kwa kosa hilo kamati imetoa onyo na faini ya Sh. milioni 5 itakayolipwa TCRA.

Leave A Reply