The House of Favourite Newspapers

Kisa kuchelewa harusini… mume adaiwa kumuua mkewe!

0

auawa (1)    Beatrice Kiriho enzi za uhai wake.

Richard Bukos na Issa Mnally, UWAZI

Dar es Salaam: Jeshi la Polisi nchini linamshikilia Fidelis Buberwa, mkazi wa Tabata jijini hapa kwa tuhuma za kumshushia kipigo mkewe, Beatrice Kiriho na kumsababishia kifo.

auawa (11)Fidelis Buberwa ambaye ni mume wa marehemu.

Bubelwa anadaiwa kumjeruhi kwa kipigo mkewe nyumbani kwake, usiku wa Juni 11, mwaka huu kilichomuacha mwanamke huyo akiwa mahututi na baadaye kukimbizwa Hospitali ya Mwananyamala kupatiwa matibabu.

auawa (3)Akiwa hospitalini hapo, Beatrice alitibiwa kwa wiki mbili mfululizo lakini hakupata nafuu yoyote, Juni 20, mwaka huu akaaga dunia kwa mateso makali.

auawa (4)Akizungumza na Uwazi kwenye ibada ya kumuombea marehemu Beatrice iliyofanyika Kanisa Katoliki la Tabata Segerea jijini hapa, kaka wa marehemu ambaye aliomba jina lake lisiandikwe gazetini, alisema wanandoa hao kabla ya tukio hilo walikuwa na migogoro ya mara kwa mara ya mapenzi iliyokuwa ikisababishwa na wivu.

auawa (5)Kaka huyo aliendelea kueleza kuwa migogoro hiyo ilikuwa ikisababisha wawili hao kupigana mara kwa mara lakini walikuwa wakisuluhishwa.

Akielezea siku ya kipigo hicho kilichosababisha kifo hicho, kaka huyo alisema:

auawa (6)“Juni 11, mwaka huu, Beatrice alikwenda kwenye harusi ya mtayarishaji wa muziki aitwaye Manecky (Emmanuel Sewando) ambaye alikuwa akifunga ndoa siku hiyo, sasa aliporudi mumewe akaanza kumfokea kwa nini alichelewa kurudi.

auawa (7)“Dada alimuelezea sababu zilizomchelewesha lakini shemeji inaonekana hakumuelewa hivyo akaanza kumshushia kipigo mpaka akawa mahututi. Kufuatia hali hiyo, wasamaria wema walimkimbiza hospitali kupatiwa matibabu mpaka umauti ulipomfika.

auawa (8)“Ukweli kifo cha dada yetu kinatupa uchungu sana, inaonesha ni kama vile alijua hawezi kupona maana akiwa hospitalini mara kwa mara alikuwa akitusisitiza tumuangalizie watoto wake watatu, ambao wa kwanza ana umri miaka minne na wengine wawili mapacha wana umri wa mwaka mmoja na miezi kadhaa,” alimaliza kusema kaka huyo.

auawa (9)Naye Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kipolisi Ilala, Kamishna Msaidizi, Salum Hamduni alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuongeza kuwa Beatrice alifikishwa Kituo cha Stakishari kama majeruhi na kupewa hati namba tatu (PF3) ya polisi kwa ajili ya kwenda kutibiwa ambapo ndugu zake walimpeleka Hospitali ya Mwananyamala ambapo alitibiwa mpaka alipopatwa na umauti.

auawa (2)“Mume wa marehemu naye alifikishwa kituoni hapo na kufunguliwa jalada la kujeruhi lakini baada ya kifo hicho jalada hilo limebadilika na kuwa la mauaji na anashikiliwa na polisi,” alisema Kamanda Hamduni.

auawa (10)Marehemu alizikwa Ijumaa iliyopita kwenye Makaburi ya Tabata Kinyerezi jijini Dar.

Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi. Amina.

Leave A Reply