The House of Favourite Newspapers

Kisa Mayele, Kocha Africain Aingia Mchecheto Kutinga Makundi Kombe la Shirikisho

0
Kocha Bertrand Marchan wa Club Africain ya Tunisia.

 

KOCHA Bertrand Marchan wa Club Africain ya Tunisia amesema kuwa anawatambua wapinzani wao kuwa ni wazuri ikiwa ni pamoja na safu ya ushambuliaji inayoongozwa na Fiston Mayele.

 

Yanga inatupa kete ya kwanza katika mchezo wa mtoano wa Kombe la Shirikisho Afrika wakisaka tiketi ya kutinga hatua ya Makundi Kombe la Shirikisho Afrika.

Fiston Mayele.

Akizungumza na Waandishi wa Habari jana jijini Dar, Marchan alisema: “Ninawatambua wapinzani wetu Yanga wana wachezaji wazuri kama Fiston Mayele. Huyu nilimfahamu tangu akiwa AS Vita (DR Congo) ambapo nilitaka kumsajili kabla sijatua hapa (Club Africain), pia Tuisila Kisinda, Jesus Moloko hawa ni mawinga wazuri niliwaona walipokuwa AS Vita.

 

“Mchanganyiko wa wachezaji wao wa kigeni umeifanya Yanga kuwa imara lakini tunahitaji ushindi kesho (leo),” alisema kocha huyo.

 

Naye nahodha wa timu hiyo, Nader Chandri, alisema kuwa wanahitaji ushindi kwenye mchezo dhidi ya Yanga ambao anaamini utakuwa na ushindani mkubwa.

Stori: Lunyamadzo Mlyuka na Issa Liponda

Leave A Reply