Kisa Mbeya Kwanza, Kocha Yanga Awaonya Wachezaji Wake Wasiwachukulie Poa

KOCHA Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi amesema kuwa amewaambia wachezaji wake wasiwachukulie poa Mbeya Kwanza ili yasije yakajitokeza kama yaliyotokea katika mchezo dhidi ya Prisons.

 

Nabi ameweka wazi kuwa timu kama Mbeya Kwanza ambazo zipo kwenye nafasi za chini hujituma zaidi haswa katika michezo ya mwisho ili zipate matokeo mazuri hivyo sio za kuzidharau.

 

Yanga leo Ijumaa wanatarajiwa kucheza na Mbeya Kwanza katika mchezo wa ligi kuu utakaofanyika katika Uwanja wa Mkapa Dar.

Na Waandishi Wetu

4232
SWALI LA LEO
YANGA/SIMBA KIMATAIFA
Baada ya usajili wa nguvu, mechi za Siku ya Wananchi na Simba Day kisha mechi ya ufunguzi wa Ligi Kuu ya Ngao ya Hisani, je, ni timu gani unaamini itafanya vizuri kimataifa?Toa comment