The House of Favourite Newspapers

Mobetto Athibitisha Kutolewa Posa ya Shilingi Milioni 10

0
Hamisa Mobetto mwanamuziki na mwanamitindo wa nchini Tanzania

HAMISA Hassan Mobetto au Misa; ni mwanamitindo, msanii wa muziki na mjasiriamali maarufu Bongo ambaye anafunguka kuwa, aliwahi kutolewa posa mara nyingi na posa ndogo ilikuwa ni shilingi milioni 10.

Hamisa amesema; “Nilishawahi kutolewa posa mara nyingi sana na wengine siwafahamu na wengine nawafahamu, lakini unakuta mambo hayajakaa sawa maana suala la ndoa ni la kujipanga.
“Posa ndogo ambayo ilishawahi kuja nyumbani ilikuwa million kumi.

Hamisa Mobetto ni mama wa watoto wawili

Mimi nina watoto na nimekuwa kwenye mazingira ya kushuhudia baadhi ya ndugu zangu wananyanyasika sababu hawana chao hivyo kabla sijaingia kwenye ndoa nataka nijikamilishe ili hata nikiingia niwe full na hata miaka ya mbele ikishindikana basi niwe na vyangu…”

Hamisa ni mama wa watoto wawili, mmoja amezaa na Mkurugenzi wa EFM na ETV, Majizzo na mwingine amezaa na staa wa muziki wa Kimataifa nchini Tanzania, Diamond Platnumz.
Cc; @sifaelpaul

Leave A Reply