The House of Favourite Newspapers

Kisa Odinga, Vituo Vikubwa vya Habari Vyafungiwa Kenya

 

BAADHI ya vituo vikubwa vya redio na televisheni vya Royal Media Services (RMS), vikiwemo runinga ya Citizen TV, vimefungiwa matangazo pamoja na kituo cha televisheni cha NTV kinachomilikiwa na kampuni ya Nation Media Group (NMG) katika baadhi ya maeneo.

 

Vituo hivyo vimekuwa vikipeperusha matangazo kuhusu sherehe iliyopangiwa kufanyika leo ya kuapishwa kwa kiongozi wa upinzani Kenya Raila Odinga.

 

Serikali ilikuwa imetahadharisha vituo vya habari Kenya dhidi ya kupeperusha moja kwa moja hafla hiyo.

Mmoja wa wahariri wakuu wa Citizen Peter Opondo amesema kwamba maafisa wa Mamlaka ya Mawasiliano ya Kenya (CA) kwamba polisi wakiandamana na polisi walivamia vituo vya kupeperushia matangazo na kuzima matangazo.

 

Citizen TV ndicho kituo cha runinga kinachoongoza Kenya. Matangazo ya kituo cha NTV yanapatikana pekee kupitia ving’amuzi vya kulipia.

Kituo kingine kikubwa KTN bado kinarusha matangazo. Fomu 34A na 34B za matokeo vituoni na katika ngazi ya maeneo bunge zilikuwa na utata wakati wa uchaguzi. Mwanamume huyu akaamua kujipamba na 34A na 34B. Na ana ujumbe pia wa Canan Direct – kuashiria matumaini ya kwenda nchi ya ahadi.

Global Publishers App imekurahisishia kutazama matokeo ya kidato cha nne kupitia simu ya mkononi. Install Global Publishers sasa uyasome yote: Bofya  au 

Comments are closed.