The House of Favourite Newspapers

KISUTU: Yaliyojiri Kortini Kesi ya Jamii Media

KESI namba 457 ya Jamhuri dhidi ya JamiiForums (inayohusu Kampuni za CUSNA Investment & Ocean Link kudaiwa kukwepa kodi katika Bandari ya Dar es Salaam, kuchonga nyaraka kutorosha makontena na kunyanyasa wafanyakazi wa kitanzania) imeahirishwa hadi Februari 15, 2018 kutokana na kukosekana kwa shahidi wa upande wa Jamhuri mahakamani hapo.

Mkurugenzi wa Jamii Media, Maxence Melo (40) na mmiliki mwenza Mike Mushi katika kesi hiyo wanakabiliwa na mashtaka ya kulizuia jeshi la polisi kufanya uchunguzi wake, kinyume na kifungu namba 22 (2) cha Sheria ya Makosa ya Mtandao Namba 14 ya mwaka 2015.

 

Watuhumiwa wanadaiwa kushindwa kutoa taarifa kuhusu mmiliki wa akaunti moja iliyosajiliwa JamiiForums huku wakijua kwamba jeshi hilo linafanya uchunguzi wa makosa ya jinai yaliyochapishwa kielektroniki kwenye tovuti hiyo.

 

Mpaka sasa mashahidi 5 wa Jamhuri wameshasikilizwa katika kesi hiyo ambayo imepigwa kalenda hadi Februari 15, 2018 kwa ajili ya kusikilizwa.

Comments are closed.