The House of Favourite Newspapers

Kisa Yanga, Simba, Azam waishangaa TFF

Ofisa Habari wa Azam, Jaffar Idd

UONGOZI wa Azam FC umeishangaa Bodi ya Ligi kwa kitendo cha timu yao kuanza kucheza mechi za mzunguko wa pili huku wakiwa na viporo vya mechi za Simba na Yanga jambo ambalo wameliita ni la ajabu katika soka.

 

Azam hadi sasa imecheza mechi 18 huku ikiwa imesaliwa na mechi mbili za mzunguko wa kwanza dhidi ya Yanga na Simba na leo Jumamosi itakuwa na kibarua mbele ya Mwadui FC mchezo ambao utapigwa katika Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar.

 

Akizungumza na Championi Jumamosi, Ofisa Habari wa Azam, Jaffar Idd alisema kuwa wao walitakiwa kucheza na Yanga kwa sasa ambao wapo hapa tofauti na Simba ambao wana majukumu mengine ya kimataifa ili mambo yaweze kwenda sawa.

 

“Timu imerejea kutoka Mapinduzi tulitarajia kuwa ratiba ingewekwa wazi juu ya mechi zetu za Simba na Yanga tutacheza lini kabla ya kuanza mzunguko wa pili lakini mambo yamegeuka tumeanza kucheza mechi za mzunguko wa pili kitu ambacho si sahihi.

 

“Tulitakiwa kucheza na timu hizo kama Yanga kwa sasa ipo hapa tulikuwa na uwezo wa kucheza nayo lakini Bodi ya Ligi wameshindwa kuweka ratiba bora hata Simba ambao hawapo hapa kutokana na michuano ya kimataifa, inabidi vyombo husika wajipange katika hili,” alisema Idd.

Comments are closed.