The House of Favourite Newspapers

Kiungo Azuiwa Kusaini Simba, Yanga

0

UONGOZI wa Namungo FC ya Ruangwa, Lindi imeanza mazungumzo na kiungo wake mshambuliaji Reliants Lusajo kwa ajili ya kumbakisha.

 

Lusajo ni kati ya wachezaji wanaowaniwa na klabu za Simba, Yanga na Azam FC. Kiungo huyo kwa mujibu wa kanuni za Fifa ni mchezaji huru kutokana na mkataba wake kumalizika mwishoni mwa msimu huu wa Ligi Kuu Bara.

 

Akizungumza na Championi Jumatatu, Mwenyekiti wa Namungo, Hassan Zidadu, alisema kuwa wameanza mazungumzo ya awali na kiungo huyo kuhakikisha anabakia kwenye msimu ujao. Zidadu alikiri kuwa kiungo huyo ni kati ya wachezaji wanaomaliza mikataba yao mwishoni mwa msimu, hivyo wamejipanga kuhakikisha wanambakisha.

 

Aliongeza kuwa wamepanga kumbakisha nyota huyo kutokana uwezo na mchango mkubwa anaoutoa kwenye timu. “Lusajo ni kati ya wachezaji wetu muhimu na tegemeo katika timu, hivyo ngumu kumuachia hivi sasa.

 

“Hivyo tupo kwenye mazungumzo naye ili kuhakikisha anabakia kwenye msimu ujao na mambo yakienda sawa ataongeza mkataba.

 

“Tumepanga kuwabakisha wachezaji wetu wote tulionao msimu huu, hiyo ni baada ya uwezo mkubwa na ushindani walioutoa msimu huu,” alisema Zidadu.

Leave A Reply