The House of Favourite Newspapers

Kiungo Mshambuliaji Aigomea Simba, Atua Jeshini

0

IMETHIBITISHWA kuwa kiungo mshambuliaji wa Simba, Hassani Dilunga amekataa ofa ndogo ya kuongeza mkataba mpya wa kuendelea kukipiga hapo huku akitajwa kurejea JKT Tanzania.

JKT inayomilikiwa na Jeshi la Kulinda Taifa Tanzania ambayo imerejea katika Ligi Kuu Bara msimu huu.Kabla aliwahi kuichezea Ruvu Shooting kujiunga na Simba aliyomaliza mkataba.

Kiungo huyo alikuwepo nje ya uwanja kwa msimu mzima akiuguza majeraha ya goti ambayo amepona baada ya uongozi wa Simba kumpeleka Afrika Kusini kwa ajili ya matibabu.

Nyota huyo yupo na timu hiyo, tangu mwezi uliopita akifanya mazoezi ya pamoja na kikosi hicho baada ya kupona kwa asilimia mia moja.

Taarifa ambazo imezipata Spoti Xtra, kiungo huyo alikuwa tayari kuongeza mkataba wa kuendelea kuichezea timu hiyo, lakini baadaye amebadili maamuzi kutokana na ofa ndogo aliyowekewa mezani.

Mtoa taarifa huyo alisema kuwa dau hilo alilopewa Simba halijamshawishi kubakia hapo, na haraka akaenda JKT Tanzania ambako walimwita na kumpa ofa nzuri ambayo ameikubali.

Aliongeza kuwa kiungo huyo atajiunga na JKT Tanzania katika msimu ujao kama mchezaji huru baada ya kumalizana na Wanajeshi hao waliopanga kurejea kwa kishindo katika ligi msimu ujao.

“Dilunga hatakuwa sehemu ya wachezaji wa Simba katika msimu ujao, ni baada ya kuchukua maamuzi ya kuondoka hapo na kwenda JKT Tanzania kusaini mkataba baada ya kushawishika na ofa nzuri aliyowekewa.

“Hakushawishika na ofa ndogo aliyowekewa na uongozi wa Simba, hivyo akaona ni bora ahondoke hapo akatafute changamoto nyingine katika msimu ujao akiwa na timu hiyo,iliyopanda msimu huu.

“Mwenyewe amepanga kurejea huko kwa ajili ya kurejesha thamani yake katika soka baada ya kupotea msimu mzima kutokana na majeraha ya goti,” alisema mtoa taarifa huyo.

Akizungumzia hilo Meneja wa Habari wa Simba, Ahmed Ally kuzungumzia hilo alisema kuwa “Hivi sasa viongozi wapo msituni wakifanikisha baadhi ya usajili wa wachezaji wakiwemo wapya na wale ambao mikataba yao inamalizika mwishoni mwa msimu huu. Hivyo tusubirie kila kitu tutaweka wazi.

STORI NA WILBERT MOLANDI

KOCHA KAZE “MCHEZO UTAKUA MGUMU, TUMEJIANDAA kwa CHOCHOTE ILI TUTINGE FAINALI CAF”

Leave A Reply