The House of Favourite Newspapers

Straika Mzambia Apewa Kazi Maalum Yanga Dhidi ya Marumo Gallants

0
Mzambia Kennedy Musonda.

KOCHA Mkuu wa Yanga Mtunisia, Nasreddine Nabi amesema kuwa hana hofu ya kupoteza mchezo wa marudiano dhidi ya Marumo Gallants ya nchini Afrika Kusini l kwa kumkosa Bernard Morrison, kwani anaye Mzambia Kennedy Musonda.

Hiyo ni katika kuelekea mchezo wa marudiano wa Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika utakaopigwa Jumatano Mei 17, 2023 kwenye Uwanja wa Royal Bafokeng ambao upo katika mji mdogo wa Phokeng, South Africa unaomilikiwa na Jamii ya Royal Bafokeng Nation.

Katika mchezo huo, Yanga wataingia uwanjani bila ya Morrison ambaye aliifungia timu hiyo, bao moja katika ushindi wa mabao 2-0 walioupata kwenye Uwanja wa Mkapa Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na Spoti Xtra, Nabi alisema kuwa anajivunia wigo mpana wa kikosi chake ambacho kinaundwa na wachezaji wengi bora na wenye viwango vikubwa vitakavyompa matokeo mazuri.

Nabi alisema kuwa katika mchezo wa kwanza, hakumtumia Musonda kiufundi akipanga kumchezesha katika pambano la marudiano huko Sauzi akijua kumkosa Morrison ambaye ana zuio la kuingia nchini huko.

Aliongeza kuwa katika mchezo ataingia uwanjani akiwa mshambuliaji ambaye hawamfahamu wapinzani wake Marumo Gallants huku akimtumia Musonda kuongoza mashambulizi katika goli la wapinzani.

“Kabla ya mchezo wa kwanza kuucheza kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar nilijua kabisa tutamkosa Morrison katika mchezo wa marudiano, hivyo nikaona nimtumie yeye kuiongoza safu ya ushambuliaji huku nikimpumzisha Musonda kwa makusudi.

“Hivyo kabla ya mchezo nilimwambia Morrison aucheze mchezo huu wa nyumbani kwa nguvu zote ili tupate matokeo mazuri kabla ya kwenda kurudiana nao Marumo Gallants kwao.

“Nashukuru alifanya vile ambavyo nilitaka, alipambana na kufunga bao hivyo kazi kubwa kamuachia Musonda ambaye anatakiwa na yeye kuipambania timu atakapoanza katika kikosi cha kwanza tutakaporudiana na Marumo Gallants,” alisema Nabi.

STORI NA WILBERT MOLANDI

KOCHA KAZE “MCHEZO UTAKUA MGUMU, TUMEJIANDAA kwa CHOCHOTE ILI TUTINGE FAINALI CAF”

Leave A Reply