The House of Favourite Newspapers

Kiungo wa Kazi Ngumu Ndani ya Kikosi cha Simba Ajifunga Miaka Miwili Kuvaa uzi Mwekundu

0
Mzamiru Yassin

 

KIUNGO wa kazi ngumu ndani ya kikosi cha Simba SC, Mzamiru Yassin, amejifunga miaka miwili kuendelea kuvaa uzi mwekundu.

 

Mzamiru ni chaguo la kwanza la Kaimu Kocha Mkuu wa Simba, Seleman Matola ambaye amempa jukumu la kuichezesha timu na kusambaza mipira mirefu kama alivyofanya kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Mbeya City.

 

Mzamiru ambaye alijiunga na Simba mwaka 2015 akitokea Mtibwa Sugar, atakuwepo hapo mpaka 2024 baada ya kuongeza mkataba hivi karibuni.

 

Taarifa ilizozipata Spoti Xtra kutoka ndani ya Simba, zimeelezwa kwamba: “Mzamiru amepewa mkataba mpya wa miaka miwili kuendelea kukipiga Simba, hiyo ni baada ya kazi yake kueleweka.”

 

Mbali na Mzamiru, pia kipa namba moja wa kikosi hicho, Aishi Manula, naye ameongeza mkataba wa miaka mitatu kuendelea kuichezea timu hiyo.

 

Manula amecheza mechi 21 kafungwa mabao 11 na hajafungwa kwenye mechi 11 akiwa hajafungwa kwenye mechi 11 baada ya kutumia dk 1,890 huku Mzamiru yeye akiwa ametupia mabao mawili na pasi mbili za mabao.

MWANDISHI WETU | GPL

WAARABU WAMEFIKA BEI SAKHO ANAONDOKA SIMBA, AZIZI KI ATUA BONGO | KROSI DONGO

Leave A Reply