The House of Favourite Newspapers

Kiungo Yanga Yupo Hoi Zanzibar

Mohammed Issa ‘Banka’.

KIUNGO mshambuliaji mpya wa Yanga ambaye bado hajafanikiwa kuonekana na uzi wa klabu hiyo, Mohammed Issa ‘Banka’ amefunguka kuwa kwa sasa yuko kwao Zanzibar akiuguza magoti.

 

Banka alisajiliwa na Yanga hivi karibuni akitokea Mtibwa Sugar, lakini mpaka sasa hajawahi kuonekana hata katika mazoezi ya timu yake hiyo mpya.

 

“Sasa hivi nipo nyumbani Zanzibar ninaumwa magoti lakini namshukuru Mungu naendelea vizuri na nimekuwa nikiwasiliana na viongozi wa timu kipindi hiki.

 

“Yanga wanajua kama naumwa na wamekuwa wakiwasiliana na mimi vyema bila tatizo na nikipona nitaonekana tu,” alisema Banka.

 

Hata hivyo, taarifa ambazo siyo rasmi zilidai kuwa sababu za kutoonekana mchezaji huyo ni kutokana na kutopewa pesa zake za usajili na Yanga.

Stori na Martha Mboma, Championi Ijumaa

Comments are closed.