The House of Favourite Newspapers

KMC Kushuka Dimba la Jamhuri Kesho Dhidi ya Dodoma jiji Michuano ya Kombe la ASFC

0
Kocha msaidizi wa Timu ya KMC FC, Habibu Kondo akitoa maelekezo kwa wachezaji wa timu hiyo wakati wa maandalizi ya mwisho kuelekea kwenye mchezo wa michuano ya kombe la shirikisho dhidi ya Dodoma jiji utakaopigwa kesho saa 16:00 jioni katika uwanja wa Jamuhuri Jijini Dodoma.

Kikosi cha KMC FC kesho kitashuka katika dimbani la Jamuhuri jijini Dodoma kwa ajili ya mchezo wa michuano ya kombe la Shirikisho ( ASFC) dhidi ya Dododma Jiji FC mchezo ambao utapigwa saa 16:00 jioni.

Mchezaji wa Timu ya KMC FC Andrew Vicent akiwa kwenye mazoezi na wenzake ya kujiandaa na mchezo wa michuano ya kombe la shirikisho dhidi ya Dodoma jiji.

 

msaidizi wa Timu hiyo, Habibu Kondo amesema kuwa tayari walishafanya maandalizi ya kutosha tangu wakiwa jijini Dar es Salaam na kwamba hana hofu katika mchezo huo licha ya kwamba michuano hiyo ni migumu lakini anakiamini kikosi chake kitakwenda kufanya vizuri na hivyo kuendelea katika hatua inayofuata ya michuano hiyo ya ASFC.

Mchezaji wa Timu ya KMC FC ,Abdul Hillary akiwa kwenye mazoezi kujiandaa na mchezo wa kesho wa michuano ya kombe la shirikisho dhidi ya Dodoma jiji.

Ameongeza kuwa timu anayokutana nayo kesho ni nzuri nakwamba imekuwa ikifanya vizuri katika michezo yake ya Ligi kuu hivyo pamoja na yote bado kama kocha na benchi la ufundi kwa ujumla watahakikisha kuwa Kino Boys inakwenda kufanya vizuri katika mchezo wa kesho.

 

“Michuano hii inafahamika kabisa kwamba ukifungwa unatoka, kwahiyo pamoja na kwamba tunakutana na timu yenye ushindani mkubwa, lakini KMC FC imejiandaa vizuri kwasababu tunahitaji kuchukua kombe hilo awamu hii, na uwezo huo tunao” amesema Habibu Kondo.

 

KMC inakutana kwa mara ya pili na Timu ya Dodoma Jiji ambao katika mchezo wa kwanza ulikuwa ni wa Ligi kuu soka Tanzania bara ambapo walicheza katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam na Kino Boys kuibuka na ushindi wa magoli mawili kwa sifuri.

Imetolewa leo Aprili 30

Na Christina Mwagala

Afisa Habari wa Timu ya KMC FC.

 

Leave A Reply