The House of Favourite Newspapers

Kocha Al ahly amkomesha Kamusoko

0

THABANI KAMUSOKOKiungo wa kimataifa wa Yanga, Mzimbabwe, Thabani Kamusoko.

Wilbert Molandi, Dar es Salaam
KIUNGO wa kimataifa wa Yanga, Mzimbabwe, Thabani Kamusoko na Pato Ngonyani, wana kibarua kigumu wakati timu yao itakapovaana na Al Ahly ya Misri.

Yanga itavaana na Al Ahly kwenye mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika itakayopigwa Aprili 9, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Timu hiyo itavaana na Waarabu hao baada ya kuwatoa Cercle de Joachim ya Mauritius kabla ya kuwaondoa APR ya Rwanda, katika hatua ya kwanza ya michuano hiyo.
Viungo hao watakutana na ugumu kwenye michezo hiyo kutokana na aina ya mfumo anaoutumia Kocha Mkuu wa Al Ahly, Martin Jol wa 4-3-2-1 akiwajaza viungo nane, mabeki wanne huku akimbakisha mbele mshambuliaji mmoja pekee raia wa Gabon, Malick Evouna.

Mfumo huo, unaonekana kuwatumia viungo watano tofauti na Yanga yenyewe inayonolewa na Mholanzi, Hans van Der Pluijm ambayo imekuwa ikitumia mfumo wa  4-3-3 akimtumia, Haruna Niyonzima, Deus Kaseke na Kamusoko.

_67440411_158257956Lakini kwenye mechi hii ya kwanza itakayochezwa Dar, Niyonzima hatakuwepo uwanjani kutokana na kutumikia adhabu ya kadi mbili za njano, hivyo kibarua kitakuwepo kwa Kamusoko, Kaseke na Pato Ngonyani, watakaopambana na viungo watano.

Kwa upande wa Niyonzima alisema: “Ni kweli Al Ahly wanatumia mfumo wa kujaza viungo kwa lengo la kudhibiti safu ya kiungo, kikubwa tunashukuru tumefanikiwa kuziona video za mechi zao, hivyo tunazifanyia kazi kuhakikisha hatuwapi nafasi ya kucheza.”
Jol aliwahi kuzifundisha klabu kubwa za Uingereza, Tottenham Hotspur, Fulham FC na AFC Ajax, kabla ya kutua Al Ahly, mwaka huu.

Leave A Reply