The House of Favourite Newspapers

Kocha AS Vita Afunguka Dili Lake Simba -Video

0
Kocha Mkuu wa AS Vita ya DR Congo, Florent Ibenge.

SIKU chache baada ya kuhusishwa kuwaniwa na Simba, Kocha Mkuu wa AS Vita ya DR Congo, Florent Ibenge amefunguka juu ya tetesi hizo huku akiweka wazi kuwa yupo tayari kwa kazi.

 

Kocha huyo amefunguka kuwa ndiyo anaweza kuwa kocha wa Simba endapo tu klabu hiyo itakuwa inamuhitaji na itafanikiwa kumpa ajira.

Hivi karibuni kumekuwa na taarifa mbalimbali zikimuhusisha kocha huyo kutakiwa na Simba kwa ajili ya kuchukuwa nafasi ya kocha wa sasa wa Simba, Sven Vandenbrorck ambaye inadaiwa anaweza kuondoka baada ya msimu kumalizika.

 

Akizungumza na Championi Ijumaakatika mahojiano maalum juu ya kuhitajika na Simba, Ibenge alisema kuwa kwa sasa bado ni tetesi na asingependa kuzungumzia hizo tetesi, lakini kama kweli wanamuhitaji yeye hana shida kwani kinachotakiwa ni Simba kufuata taratibu za masuala ya kimkataba.

 

“Mimi ni kocha mkubwa nisingependa kuzungumzia kuhusu tetesi zinazonihusu mimi kuhitajiwa na Simba, kuifundisha timu hiyo inawezekana lakini kama wao wananihitaji wanatakiwa kufuata taratibu zote.

 

“Simba ni timu nzuri katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati nakumbuka ilitufunga kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika, naamini wanamipango ya kufika mbali,” alisema kocha huyo.

STORI: MARCO MZUMBE, Dar es Salaam

Leave A Reply