The House of Favourite Newspapers

Kocha As Vita Amtanguliza Mumbere Simba

0

 MEFICHUKA rasmi kuwa Kocha wa AS Vita ya DR Congo, Florent Ibenge yupo karibu kutua ndani ya Simba hiyo ni kutokana na kumshawishi kiungo wa timu hiyo, Jeremy Mumbere kujiunga Simba badala ya timu nyingine zinazomuhitaji.

 

Mumbere anayecheza katika eneo la kiungo, amekuwa akihusishwa kutakiwa na Simba ambao wanahitaji kukiongezea nguvu kikosi chao kwa ajili ya michuano ya kimataifa msimu ujao.

 

Kitendo cha kocha huyo kumshawishi Mumbere kujiunga na Simba kinaonyesha kuwa ni wazi kocha huyo yupo kwenye mipango ya kujiunga Simba ndiyo maana anamtanguliza mchezaji wake ili wakaungane kwa pamoja hapo baadaye kama na yeye atafanikisha dili lake.

Akizungumza na Championi Jumamosi, Mumbere alisema kocha Ibenge amekuwa akimshawishi kujiunga na Simba na siyo timu zingine ambazo zimepeleka ofa ya kuhitaji saini yake.

 

“Kuna timu nyingi zimeonyesha nia ya kuhitaji kunisajili ambazo nyingi ni kutoka Afrika lakini kocha wangu amekuwa akinishawishi nijiunge na Simba kuliko timu yoyote.

 

“Lakini kuhusu mimi kujiunga na Simba ni kweli kwa tulipofikia tupo katika hatua nzuri ya kukamilisha usajili hivyo kama mambo yataenda kama yalivyopangwa nitakuwa mchezaji wa Simba hivi karibuni,” alisema kiungo huyo.

Stori: Marco Mzumbe, Dar es Salaam

Leave A Reply