The House of Favourite Newspapers

Kocha Man United Amsifia Cristiano Ronaldo

0

BOSI wa Manchester United, Ralf Rangnick amefunguka juu kiwango ambacho alionyesha staa wake, Cristiano
Ronaldo dhidi ya
Brighton akisema ni bora kushuhudia tangu atue kikosini hapo.


Rangnick
ameanza kuifundisha Man United mwishoni mwa Desemba mwaka jana, baada ya Ole Gunnar Solskjaer kuondolewa.


Man United juzi,
ilishinda kwa mabao 2-0 dhidi ya Brighton mchezo ambao ulipigwa katika Dimba la Old Trafford ukiwa na Premier League.


Katika mchezo huo,
Ronaldo alifunga bao na kufuta ukame kwani alikuwa amecheza mechi sita mfululizo bila kufunga.

 

Rangnick alisema alivutiwa na kiwango cha Ronaldo kwani kilikuwa bora kuliko kawaida tangu atue kikosini hapo na kuanza kuinoa timu hiyo.


“Kiwango cha
Cristiano kilikuwa bora sijapataona tangu nimekuwa naye hapa na alikuwa bize akishirikiana na wenzake kuona kila kitu kinaenda sawa.


“Nafikiri
hata wiki iliyopita alikuwa bora ila sio kwa kiwango hiki na ndiyo maana ni mchezaji muhimu kwenye kikosi chetu.

 

“Kitu muhimu sio kufunga tu bali amefunga bao zuri na bora ambalo lilikuwa muhimu kwetu
kama timu jambo ambalo ni
muhimu na tumefanikiwa kuondoka na clean sheet,” alisema.

Leave A Reply