The House of Favourite Newspapers

Kocha Mkuu Simba Atangaza Pointi 15 Za Ubingwa

0

MARA baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mashujaa katika mchezo wa Ligi Kuu Bara uliopigwa juzi Jumamosi, Kocha Mkuu wa Simba, Abdelhak Benchikha ametamba kujipanga kuzoa pointi zote 15 za michezo yao mitano ijayo ili kujiweka kwenye nafasi nzuri ya kuwa mabingwa.

Simba juzi Jumamosi ilifanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0, bao ambalo limewafanya wafikishe pointi 26 na kuzidi kupunguza pengo la pointi wakikamatia nafasi ya tatu kwenye msimamo.

Mara baada ya mchezo huo dhidi ya Mashujaa, sasa Simba wanatarajiwa kuwa na michezo mitano mfululizo ya Ligi Kuu Bara kabla ya kurejea kwenye ratiba ya michezo ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Akizungumza na Championi Jumatatu, Benchikha alisema: “Tumefurahi kuanza kwa matokeo ya ushindi katika mchezo huu dhidi ya Mashujaa ambao ni wazi ulikuwa mchezo mgumu, nawapongeza wachezaji na benchi la ufundi kwa kuendelea kupambana.

“Tuna ratiba ngumu ya michezo mitano mfululizo ijayo ambayo malengo yetu ni kuhakikisha tunashinda yote na kuvuna pointi 15 ili kujiweka kwenye nafasi nzuri ya kushindania ubingwa kwa kuwa ni ukweli kuwa unapovuna pointi nyingi kwenye ratiba ngumu kama hii basi inaongeza ari ya kupambana.”

Stori na Joel Thomas

MTIFUANO MKALI BUNGENI: LAMBERT AMNYOOSHEA KIDOLE OLE SENDEKA – “UNAJITETEA – HUENDA ULIIBA KURA”…

Leave A Reply