The House of Favourite Newspapers

Kocha Mpya Simba Akabidhiwa Kiungo, Viongozi Watia Neno

0
David Udoh Kiungo Mnigeria aliyefanikiwa kufanya majaribio na Simba SC msimu huu

WAKATI Simba SC ikiwa kwenye mchakato wa kumsaka kocha mpya atakayerithi mikoba ya Pablo Franco, imeelezwa kwamba, ataanza na suala zima la usajili, huku jina la kiungo mkabaji Mnigeria, David Udoh, likiwa mezani likimsubiri.

 

Udoh ambaye Januari, mwaka huu alikuja kufanya majaribio kikosini hapo akicheza michuano ya Kombe la Mapinduzi, anatajwa kuchukua nafasi ya Taddeo Lwanga.

 

Mei 30, mwaka huu, Simba ilitangaza kuachana na Pablo raia wa Hispania ambaye alijiunga na timu hiyo Novemba 2021.

Kocha Brandon Truter wa Amazulu ya Afrika Kusini anahusishwa kuchukua mikoba ya Pablo Franco Martin

Kwa mujibu wa taarifa ambazo imezipata, Spoti Xtra kutoka kwa mmoja wa mabosi wa Simba, wamepanga kumsajili kiungo huyo baada ya kuvutiwa na kiwango chake alichokionesha katika Kombe la Mapinduzi.

 

“Upo uwezekano mkubwa wa Udoh kupewa mkataba wa kuichezea Simba katika usajili ujao katika kukiimarisha kikosi chetu.

 

“Uongozi na benchi la ufundi ulivutiwa na kiungo huyo tangu usajili wa dirisha dogo, lakini ilishindikana kumsajili kutokana na idadi ya wachezaji 12 wa kimataifa kukamilika.

 

“Hivyo tukakubaliana kumsajili katika usajili wa dirisha kubwa baada ya kutoa nafasi kwa wachezaji waliopo kuona viwango vyao akiwemo Lwanga ambaye alikuwa katika majeraha, lakini ameonekana bado ana changamoto,” alisema bosi huyo.

Mohammed Adil Erradi anatajwa kuwa moja ya makocha wanaowa niwa na Simba SC

Akizungumzia hilo, Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally, alisema: “Suala hilo la usajili hivi sasa tumelisimamisha, tunamsubiria kocha mpya atakayekuja ndiye atasimamia usajili wote.

 

“Kocha huyo mpya ndani ya wiki mbili hizi atajulikana na kumtambulisha katika vyombo vya habari, lengo ni kuepukana na visingizo kutoka kwa makocha hao wamekuwa wakijitetea kutofanya usajili timu inapopata matokeo mabaya.”

 

Baadhi ya makocha wanaotajwa kuhusishwa na Simba ni Mohammed Adil Erradi raia wa Morocco anayeifundisha APR ya Rwanda na Msauzi, Brandon Truter wa Amazulu ya Afrika Kusini.

WILBERT MOLANDI NA MUSA MATEJA

Leave A Reply