The House of Favourite Newspapers

Kocha mpya Simba Apewa Mamilioni ya Usajili

0

MAMBO ni moto Simba, hivyo ndivyo unavyoweza kusema baada ya uongozi wa Simba kutenga mamilioni ya usajili ambayo atakabidhiwa kocha mpya wa timu hiyo ambaye atatambulishwa keshokutwa Jumatano katika kipindi hiki cha dirisha dogo.

 

Uongozi huo chini ya mwekezaji, Mohammed Dewji ‘Mo’ umetenga Sh milioni 76 kwa ajili ya usajili ambazo itazitumia katika dirisha dogo litakalofunguliwa Desemba 16, mwaka huu.

 

Haya yamesemwa jana na uongozi wa timu hiyo katika mkutano mkuu wa wanachama wa klabu hiyo uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

 

Mhasibu wa Simba, Mathiew Asunga, akisoma mapato na matumizi ya klabu hiyo katika mkutano huo, alisema kuwa wametenga kiasi hicho cha Sh milioni 76 kwa ajili ya kukiimarisha kikosi cha timu hiyo katika kipindi hiki cha dirisha dogo.

 

“Bajeti ya msimu huu ni Sh bilioni 6.188 ambapo katika hiyo mapato ni bilioni 5.814 na matumizi ni bilioni 6.188 kukiwa na upungufu wa milioni 373.

 

“Hapo kuna mishahara ambapo ni bilioni 4.16 lakini kuna fedha za masoko milioni 52.4 na kuna maendeleo ya timu 241 na matumizi mbalimbali ni mil 123,” alisema Asunga.

Hadi sasa kocha anayepewa nafasi kubwa zaidi kuchukua mikoba hiyo ni Mzambia, Beston Chambeshi kama ambavyo Championi limekuwa likiripoti.

IBRAHIM MUSSA | Dar es Salaam

 

Leave A Reply