The House of Favourite Newspapers

Kocha mpya Yanga Afunguka Kiwango cha Metacha, Shikalo

0

AKIANZAkibarua cha kukinoa hicho, Kocha Mkuu wa makipa wa Yanga raia wa Kenya. Razack Siwa amesema kuwa amevutiwa na viwango vya makipa wote aliowakuta.

Kauli hiyo aliitoa mara baada ya kocha huyo kuanza kibarua cha kukinoa kikosi hicho juzi Jumatatu kwenye kambi ya timu hiyo iliyoweka kijiji cha Avic Town, Kigamboni nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.

 

Safu ya magolikipa wa Yanga hivi sasa inaundwa na kipa raia wa Kenya, Farouk Shikalo, Metacha Mnata na kinda Ramadhani Kabwili.

Akizungumza na Championi Jumamosi,Siwa alisema kuwa magolikipa aliowakuta wana uwezo mzuri jukumu lake yeye hivi sasa ni kuwasaidia kuondoa changamoto zinazowakabili wawapo golini.

 

Siwa alisema kuwa kabla ya kujiunga na Yanga alikuwa akiwafuatilia kwa ukaribu magolikipa wote tofauti na Shikalo ambaye yeye anafahamu uwezo tangu anamfundisha akiwa Bandari FC ya nchini ya Kenya.

 

Aliongeza kuwa vipo vitu vichache vya kuwaongezea makipa hao mara baada ya kuwaona katika mazoezi ya wiki ambavyo vipo chini ya uwezo anaamini watakuwa bora golini.

 

“Bado nina imani kubwa na Yanga katika mbio za ubingwa katika msimu huu na hiyo ni kama tutaungana kwa pamoja kwa kuanzia benchi la ufundi, wachezaji, viongozi na mashabiki.

 

“Mimi kama kocha wa makipa nitatimiza majukumu yangu ya kuwandaa magolikipa wangu kwa kuwapa mbinu nzuri zitakazozuia mabao kuingia wavuni kwetu.

 

“Kwani sina hofu na makipa niliowakuta Yanga, kila mmoja ana uwezo mkubwa, kuna vitu ambavyo wanavikosa na mara nyingi nimepata kushuhudia mechi walizocheza na kuona makosa wanayoyafanya, nina imani nitawasaidia na kufikia malengo yetu,” alisema Siwa.

STORI: WILBERT MOLANDI, Dar es Salaam

Leave A Reply