The House of Favourite Newspapers

Kocha Mtibwa: Pointi ya Yanga Itatupa Ubingwa

0

BAADA ya vinara wa Ligi Kuu Bara, Mtibwa Sugar kuwang’ang’ania kooni mabingwa watetezi, Yanga na kuwalazimisha suluhu, Kocha Mkuu wa Mtibwa, Zuberi Katwila, amefunguka kuwa pointi moja ambayo wameipata kwa wapinzani wao hao itawasaidia kwenye harakati zao za kuchukua ubingwa.

 

Jumamosi iliyopita, Mtibwa Sugar wakiwa ugenini kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar waliwalazimisha suluhu Yanga wakiwa chini ya kocha wao, George Lwandamina. Matokeo hayo yanawafanya Mtibwa kuwa na pointi 11 huku Yanga wakifikisha tisa kwenye msimamo wa ligi.

 

Akizungumza na Championi Jumatano, Katwila amesema kwao kuambulia pointi moja kwa Yanga ni jambo la kujipongeza kutokana na wapinzani wao kuwa na kikosi ambacho kimefanya usajili mkubwa msimu huu, ambapo pointi hiyo waliyopata itakuwa msaada mkubwa kwao katika kuelekea kutimiza ndoto yao waliyojiwekea kwa msimu huu.

 

“Kwangu mimi sijapenda matokeo haya kwani tulikuja hapa tukiwa na nia ya kutaka kushinda lakini siyo mbaya tumepata pointi moja ambayo imetuongezea nafasi ya kupambana zaidi kuelekea kutwaa ubingwa jambo ambalo tumejiwekea kwa msimu huu na tunataka kulifanikisha suala hilo.

 

“Kupata matokeo haya mbele ya Yanga ambayo imetumia kiasi kikubwa cha fedha kwenye usajili siyo jambo la kawaida, lakini kwetu tumelifanikisha na sasa tunaangalia michezo yetu ijayo kuhakikisha tunashinda baada ya kupita mechi hizi mbili ambazo tumeambulia pointi mbili pekee,” alisema Katwila.

Lema, Nassari, Msigwa Watinga Takukuru na Ushahidi

Leave A Reply