The House of Favourite Newspapers

Kocha Mualgeria Akabidhiwa Taifa Stars Achukua Mikoba ya Kim Poulsen

0
Adel Amrouche

SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF), limemtangaza Adel Amrouche kuwa Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars.

Kocha huyo raia wa Ubelgiji mwenye asili ya Algeria, ana uzoefu mkubwa na soka la Afrika baada ya kufundisha klabu na timu za taifa Ukanda wa Kusini, Mashariki, Kati na Kaskazini.

Amrouche amewahi kuwa Kocha Bora wa Afrika Mashariki mwaka 2013 wakati akiinoa Timu ya Taifa ya Kenya maarufu Harambee Stars na kuipa ubingwa wa CECAFA, kabla alifika nusu fainali mara mbili akiwa na Burundi. Akiwa Harambee Stars, ana rekodi ya kucheza mechi 20 bila ya kupoteza.

Kocha huyo mwenye miaka 58, amewahi kuzinoa timu za taifa za Equatorial Guinea, Botswana, Libya na Yemen, huku pia akipita katika klabu za RC Kouba, USM Alger na MC Algiers, zote za Algeria.

Kule DR Congo akiwa na kikosi cha DC Motema Pembe, aliiwezesha timu hiyo kubeba ubingwa wa Ligi Kuu ya DR Congo mara mbili na taji la DRC Super Cup.

Aidha kocha huyo ni mkufunzi wa walimu wa Pro Licence wa Shirikisho la Soka Ulaya (UEFA) akizalisha makocha wengi bora barani Afrika.

Kocha huyo amechukua mikoba ya Kim Poulsen raia wa Denmark ambaye aliachana na kikosi hicho Agosti, mwaka jana. Baada ya Kim kuondoka, nafasi yake ilishikiliwa kwa muda na Mzambia, Honour Janza.

STOLU NA OMARY MDOSE

HUU HAPA UKWELI WOTE KUHUSU FEI TOTO DHIDI ya YANGA na SHERIA ya FIFA ya KUVUNJA MIKATABA….

Leave A Reply