The House of Favourite Newspapers

Kocha Simba Afunguka Pacha ya Bocco, Mugalu

0

KOCHA Msaidizi wa Simba, Selemani Matola, amefunguka kwamba benchi la ufundi wanakoshwa na aina ya pacha ya washambuliaji wao, John Bocco na Chris Mugalu.

 

Kocha huyo ameongeza kwamba wanafurahishwa na mwenendo wa wawili hao kwa kuwa wamekuwa wanafunga mabao muhimu katika mechi za timu hiyo.

Bocco na Mugalu wamekuwa wakianza kwa pamoja katika mechi nne mfululizo za mashindano yote kuanzia kwenye mechi dhidi ya Kaizer Chiefs, Dodoma Jiji, Namungo FC na Ruvu Shooting.

 

Matola amesema: “Tulianza na wawili hao katika mechi na Ruvu kwa ajili ya kufunga, na kweli tukafunga mabao muhimu kwa ajili ya timu kisha baadaye tukamtoa mmoja na kuingiza kiungo.“Lakini siyo hao tu kwa kuwa tuna kikosi kipana tumekuwa na pacha nyingi katika timu, na wakicheza wanakuwa wanacheza vizuri jambo ambalo ni faida kwetu.”

Stori: Said Ally, Dar es Salaam

Leave A Reply