The House of Favourite Newspapers

Kocha Simba Akubali Chama Atue Simba

0

VIDEO tatu ambazo amepewa Kocha Mkuu wa mpya wa Simba Mhispania, Franco Pablo zimetosha kumshawishi kumrejesha kiungo mshambuliaji fundi Mzambia Clatous Chama.


Hiyo ikiwa ni siku chache
tangu kocha huyo apewe jina la kiungo huyo ambaye inadaiwa ameomba kurejea katika timu hiyo baada ya kukosa furaha katika klabu yake mpya ya RS Berkane ya nchini Morocco.

 

Chama alijiunga na Berkane katika msimu huu baada ya Simba kumuuza kwa dau la Sh 1Bil akisaini mkataba wa miaka miwili.

Kwa mujibu wa chanzo cha habari kutoka ndani ya Benchi la Ufundi la timu hiyo, kocha huyo aliomba kutazama video hizo za michezo iliyopita akiwa Simba kwa lengo la kujiridhisha uwezo wake.


Chanzo hicho kilisema
kuwa video zilitosha kumshawishi Pablo na kuomba kiungo asajiliwe haraka kama uongozi
utakuwa na mkwanja wa kutosha kuvunja mkataba Berkane.


Kiliongeza kuwa kocha
huyo alisema kwa kiwango ambacho kiungo huyo kinatosha kabisa kuingia moja kwa moja katika mfumo uchezaji.


“Kocha Pablo alisikia
tetesi za kiungo huyo kutajwa kurejeshwa katika timu, hivyo aliomba video za michezo mitatu ambayo Chama amecheza akiwa na Simba.


“Kikubwa alitaka
kujiridhisha kwa ajili ya kuangalia uwezo wake na kama ataweza kuingia katika mfumo wake na aina ya uchezaji wa soka la pasi hasa timu ikiwa na mpira.


“Baada ya kuziangalia
video hizo kocha akapendekeza kurejeshwa kwa Chama kama watakuwa na fedha za
kuvunja mkataba wake
huko anapocheza,” alisema mtoa taarifa huyo.


Akizungumzia hilo,
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba, Salim Abdallah ‘Try Again’ alisema kuwa:
“Chama hapa ni nyumbani
muda wowote atarejea, kwani hakuondoka kwa ubaya na sisi ndiyo tulimuuza.

 

Kikubwa usajili wetu tunaufanya kwa kupitia mapendekezo ya kocha wetu, hivyo kama akimuhitaji basi tutamrejesha kikosini.”

Stori na Wilbert Molandi na Musa Mateja

Leave A Reply