The House of Favourite Newspapers

Kocha Simba Awakomalia Mastaa Simba

0

KOCHA Pablo Franco amegundua kuna tatizo kubwa kwa wachezaji wake ndani ya kikosi cha Simba kushindwa kutumia vema mipira ya kutengwa ambayo ni penalti, kona na faulo.


Raia huyo wa Hispania,
tangu atambulishwe Simba Novemba 8, 2021, ameshuhudia wachezaji wake watatu, Erasto Nyoni, Bernard Morrison na Rally Bwalya wakikosa penalti katika mechi tatu tofauti.


Nyoni alikosa penalti dhidi
ya Ruvu Shooting wakati Simba ikishinda 3-1, huku Bwalya akikosa kwenye mchezo ambao Simba ilishinda 2-1 dhidi ya Azam FC.

Morrison alikosa dhidi ya Red Arrows kwenye Kombe la Shirikisho Afrika wakati Simba ikishinda 3-0.


Awali John Bocco naye
alikosa dhidi ya Biashara United kwenye mchezo uliomalizika kwa timu hizo kushindwa kufungana. Wakati huo kocha alikuwa Didier Gomes. Juzi Jumapili wakati Simba ikijiandaa na mchezo wa nusu fainali wa Kombe la Mapinduzi dhidi ya Namungo FC, kocha huyo kwenye mazoezi ya mwisho yaliyofanyika viwanja vya Mau B, Unguja, alitumia muda mwingi akiwa na mastaa wake akiwakomalia kufanya kwa usahihi zoezi la kufunga penaltina kumalizia mipira ya faulo.

 

Bwalya na Bernad Morrison, ndiyo waliokuwa wakitumika kupiga mipira ya faulo, huku Sadio Kanoute, Meddie Kagere na wachezaji wengi wa safu ya kiungo na ushambuliaji, wakisisitizwa kwenda kumalizia kwa usahihi.


Pablo aliwachagua wachezaji
11 kupiga penalti ambapo Kagere, Jonas Mkude, Morrison, Mzamiru Yassin, Chris Mugalu, Rally Bwalya, Pape Sakho na Shomari Kapombe ambao wote walifunga.

 


Huku Mohamed Hussein,
Sadio Kanoute na Kibu Denis wakishindwa kufunga ambapo Pablo alionekana kuwafokea sana.


Katika zoezi lingine, Pablo
aliwaambia mastaa wake kukaa eneo la boksi kushambulia mipira ya kona. Hali ikiwa hivyo, wapo waliofunga na wengine wakikosa ambapo pindi ikitokea mambo yamekwenda ndivyo sivyo, Pablo alionekana kuwa mkali. Mazoezi ya Simba kwa jumla yalitumia takribani dakika 120 hadi kukamilika kwake.

STORI NA ISSA LIPONDA | SPOTI XTRA

Leave A Reply