The House of Favourite Newspapers

Msukuma Achukua Fomu Kumrithi Job Ndugai – Video

0

MBUNGE wa Geita Vijijini (CCM), Joseph Kasheku ‘Msukuma’ leo Jumanne Januari 11, 2022  amechukua fomu ya kuomba kuteuliwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kugombea nafasi ya Spika wa Bunge la Tanzania katika ofisi ndogo za CCM Lumumba jijini Dar es Salaam.

 

Hatua hiyo inakuja baada ya aliyekuwa Spika wa Bunge hilo, Job Ngugai kujiuzulu Januari 6 mwaka huu.

 

Jana wakati akitoa taarifa ya waliochukua fomu, Msaidizi Mkuu Idara ya Oganaizesheni CCM Taifa, Solomon Itunda alisema mpaka jana jioni wanachama tisa walikuwa wameshachukua fomu.

 

Alisema kuwa upande wa Ofisi ya chama Dodoma waliojitokeza ni pamoja na; Dk Simon Ngatunga, Tumsifu Mwasamale, Merkion Ndofi, Dk Tulia Ackson, Godwin Kunambi na Abwene kajula.

Wengine ni Patrick Lubano, Stephen Masele na Hamidu Chamani kutoka ofisi ndogo Dar es salaam ambapo kwa upande wa Zanzibar hakuna aliyejitokeza kuchukua fomu.

Leave A Reply